UNCONFIRMED:Kauli ya Al-Shabaab Kuhusu Kuishambulia Tanzania

Taarifa kutoka redio YARAT FM ya Somalia leo saa mbili asubuhi kwenye kipindi cha MAKHAR TWALLIB:




Mkuu wa kikundi cha Al - Shabaab leo asubuhi wakati akihojiwa juu ya taarifa zilizoenea kwamba wana mpango wa kuvamia Tanzania amesema haya yafuatayo;

Kamwe hawajawahi kufikiria kushambulia, Tanzania Kwa sababu hawana sababu ya kufanya
hivo!

Amesema kwamba mbali ya kuzingatia kuwa, Tanzania kuna waislam wengi, bali pia wanajua na kutambua msaada wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1995 alipotoa msaada wa tani 500,000 za Mahindi kipindi nchi hiyo ina janga la njaa. Hivyo hawawezi kulipa unyama huo kwa marehemu baba wa taifa.

Pia kiongozi huyo aliongeza kuwa Tanzania haijapeleka jeshi lake Somalia yenyewe nchi kama nchi, tofauti na Kenya na Uganda.

Wanajeshi wachache Watanzania walioko Somalia ni katika jeshi la AU, na sio Kwa amri ya Tanzania.




Kiongozi huyo pia katoa pole katika muda wa siku mbili ambao Watanzania hususani wanachuo waliokuwa katika hali ya sintofahamu na pia vyombo vya usalama ambavyo vililazimika kuimarisha ulinzi katika sehemu nyeti mbalimbali.

Kiongozi huyo kamaliza kwa kusema kwamba wao wanazingatia msemo wa Quran kwamba, "Fight those who fight you, spare those who don't fight you''

Kutoka Mogadishu ni mimi,

Professor kilaza
Source Jamiiforums