Ndege hiyo ilikuwa isafirishe askari wajulikanao kama ‘GSU Recce’ kwenda Garissa siku ya Aprili 7, ambapo ilikuja kuonekana kwenye mtandao wa Instragram picha ya mmoja wa mabinti wa Mbiti wakiwa kwenye ngazi za ndege hiyo na maneno yaliyoandikwa: "Mombasa ni raha tu". Maneno mengine yaliyokwenda sambamba na picha hiyo yalikuwa ni: "Hi Mombasa...#birthdayweekend".
Mkuu wa jeshi la polisi (IGP), Joseph Boinnet, alikuwa amesema awali kwamba ndege hiyo haikuwepo ili kupeleka askari huko Garissa na amesema uchunguzi umeanzishwa ili kufahamu ndege hiyo ilikuwa wapi wakati magaidi wakiua wanafunzi 147.