Shamsa Ford Akana Kata Kata Kutoka na Nay wa Mitego Kimapenzi

Msanii  wa  Filamu  Nchini, Mwanadada  Shamsa Ford  amekana  kuwa  na  uhusiano  wa  kimapenzi  na  mwana  hip hop,Elibarik  Emamanuel 'Nay wa Mitego'  na  kuweka  wazi  kuwa  wako  mbioni  kuachia  filamu  yao  mpya  ya  Manyaunyau.

Akizungumza  na  mtandao  huu  juzi,Shamsa  alisema, kinachoendelea  kwa  sasa  kwenye  mitandao  ya  kijamii  ni  Promosheni  kwa  ajili  ya  ujio  wa  filamu  hiyo  waliyoshirikiana,iliyopangwa  kutoka  mwanzoni  mwa  mwezi Mei mwaka  huu.




"Hatuna  uhusiano  wa  namna  hiyo  zaidi  ya  uhusiano  wa  kikazi, kwani  tumeshirikiana  kuandaa  filamu  yetu  itakayofahamika  kwa  jina  la  Manyaunyau  na  tupo  katika  hatua  za  mwisho  kabisa  na  mashabiki  wakiiona  ndo  wataamini  nini  kilikuwa  kinaendelea  kati  yetu," alisema.


Alisema  jina  la  filamu  hiyo  limetolewa  na  Nay  mwenyewe  kutokana  na  aina  ya  filamu  yenyewe  ambayo  inalenga  familia 7 zinazoishi  katika  mvurugano,zikiwa  kwenye  maisha  ya  hali  ya  kati.