Chanzo makini kinachofahamu kwa undani kinachoendelea baina ya mastaa hao wawili, kimelidokeza gazeti hili kuwa tukio hilo lilijiri wakati wakielekea katika shughuli za mazishi ya muasisi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge aliyezikwa kijijini kwao Mkuyuni mkoani humo, ambako watu wengi maarufu walihudhuria.
“Si unajua mastaa kibao walikuwepo kwenye ule msiba, basi Rose na Shetta nao walikuwepo na wakati wa kwenda Mkuyuni, walipanda gari la Shetta hadi Morogoro mjini ambako walichukua chumba na kulala wote hadi kesho yake walipohudhuria mazishi na kurejea Dar es Salaam,” kilisema chanzo hicho.
Ili kushibisha maelezo yake, mtoa habari huyo alilitumia gazeti hili video ya wawili hao wakiwa ndani ya gari la Shetta inayomuonyesha Rose akiimba nyimbo mbalimbali za mkali huyo anayetamba na kibao chake kipya cha Shikorobo ambacho video yake imefanywa na mtayarishaji anayetamba nchini kwa sasa, Godfather wa Afrika Kusini.
Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja kama uhusiano wa wawili hao ni wa siku nyingi au umeanza hivi karibuni, ingawa gazeti hili linafahamu kuwa Shetta ni mume wa mtu akiwa amezaa naye mtoto mmoja.
Amani lilimtafuta Shetta na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu yake ya mkononi na aliposomewa mashtaka, kwanza alicheka na kusema kuwa ni kweli alikuwa msibani na alirejea Dar akiwa na Rose katika gari lake.
“Ninachoweza kusema ni kuwa ni kweli nilimpa lifti Rose wakati tunaenda kwenye mazishi ya Bonge. Kulikuwa na magari mengi ambayo mtu yeyote angeweza kupata lifti na ni kweli pia tulilala Morogoro, ilikuwa ni hoteli moja lakini kila mtu alilala chumba chake, siwezi kujihusisha na hayo mambo, mimi nina familia,” alisema msanii huyo ambaye pia aliwahi kutamba na kibao cha Kerewa, alichomshirikisha Diamond.
Kwa upande wake, Rose Ndauka alipoulizwa kuhusu suala hilo, kwanza alishtuka na kuuliza zilikopatikana habari hizo kabla ya kukiri ukweli kuwa alipanda gari la Shetta na wote kulala hoteli moja mjini Morogoro, lakini kila mtu na chumba chake.
“Halafu nisingependa kuandikwa andikwa kila siku kwa mambo hayo, unajua kama mimi nina mtu wangu? Andikeni halafu tutaonana mahakamani, maana naona lengo lenu ni kuniharibia,” alisema Rose.
credit: Global Publishers