Mkwere awatolea uvivu wasanii wenzake, asema haogopi kurogwa.

Hemed Maliyaga
Mkwere Orijino mchekeshaji wa Komedi Swahilihood.




MCHEKESHAJI mahiri katika tasnia ya filamu Swahilihood Hemed Maliyaga ‘Mkwere Orijino’ amesema kuwa anaposema ukweli haogopi kurogwa kwa sababu anaamini anachokisema ni kwa ajili ya kuweka sawa kama ni rafiki au mwigizaji mwenzake akienda tofauti.

Hemed Maliyaga
Mkwere Orijino akiwa katika pozi matata.
Hemed Maliyaga
Mkwere Original katika pozi.
“Mimi nasema tu, siogopi kurogwa bwana utaniroga wewe mimi narogwa na watanzania wengi ninaowafurahisha kila siku, nasema wasanii tubadilike katika kujitenga katika matukio kama maradhi, misiba na sherehe tushirikiane tupendane,”anasema Mkwere.
Mkwere alisema hayo wakati akiongelea suala la baadhi ya wasanii kujitenga na wasanii wenzao kwa mitazamo ya kipato, au makundi makundi ambayo kwake haoni kama yana nafasi katika maisha ya wasanii wa filamu na komedi ambao siku ya siku wote ni kitu kimoja kwani hawana tofauti sana kiubinadamu.