Tukio moja lilimeibua hisia kubwa kwa wakazi wa kijiji cha Isyongo kaunti ya nyamira nchini Kenya, baada ya Polisi kufukua maiti ya msichana mmoja Feidhi Omega 21, iliyokuwa imezikwa chini ya uvungu wa kitanda.
Taarifa zinasema kuwa binti huyo alimtembelea mpenzi wake wiki mbili zilizopita lakini hakurudi nyumbani kwao ndipo mama yake alipoanza kumtafuta na kuelekezwa kwa mpenzi wake Daniel Nyabuti, huku akiwa na matumaini ya kumkuta mtoto wake akiwa hai, walipofika nyumbani kwa kijana huyo Polisi walianza kumtafuta na kukuta kaburi chini ya uvungu wa kitanda kwa kijana huyo ambako binti huyo alikuwa amezikwa.
“Nikasilia slipaz zimepatikana kwa njia ya huyo kijana baada ya hapo kufika tarehe karibu tano hivi mwezi wa tatu nikachukua wazee wa nyumbani kuja hapa tulikuwa watatu tukakuja mpaka nyumbani kwa kijana kuuliza huyo mtoto” Moraa mama wa marehemu
Hata hivyo haikuweza kujulikana kilichotokea na kusababisha kifo cha binti huyo ingawa majirani wamesema walisikia akipiga kelele mtuhumiwa huyo amekamatwa ili kujua chanzo cha kifo hicho.
Unaweza kutazama taarifa hiyo hapa iliyoripotiwa na kituo cha K24 kwa kubonyeza play hapa chini…
bofya hapa chini kuona alivyokua akimzika>>>