Wachungaji nao waandamana kwa LOWASA kumtaka Agombee URAIS






Lowassa




Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akimkaribisha mratibu wa msafara wa wachungaji mbalimbali wa Makanisa ya Pentekoste kutoka maeneo mbalimbali nchini, Mchungaji Bernedict Kamzee kutoka kanisa la Glory of Crist la mkoani Katavi.

Mchungaji Benedickto Kamzee kutoka Kanisa la Glory of Christ la Katavi amesema wamefikia uamuzi huo wa kuja Dodoma kuonana na Edward Lowassa bila kushinikizwa wala kushawishiwa na mtu yeyote.

“Hakuna aliyetushawishi, hata siyo maaskofu wetu, hili suala halina msukumo wowote zaidi ya msukumo wa Mungu,” alisema Kamzee.




Kamzee alisema wachungaji hao wanatoka kwenye madhehebu ya EAGT, TAG, PEFA, KLPT kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza  baada  ya kuwakaribisha  Wachungaji  hao, Lowassa amepinga tuhuma zilizotolewa na baadhi ya watu kwamba amekusanya makundi ya kumuunga mkono huku akidai hana sababu ya kufanya hivyo na hana uwezo wa kuwagharamia watu hao wanao muunga mkono