Kesi hiyo imesikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Marry Moyo ambaye amesema amepokea hati ya kumfutia dhamana Sheikh Ponda kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kwa mamlaka aliyonayo hivyo yeye hana mamlaka ya kuikataa hati hiyo.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Januari 26 na 27, mwaka huu itakaposikilizwa tena.