Guus Hiddink: "Louis van Gaal analeta judo uwanjani"

 Hiddink Chelsea
Louis van Gaal alianguka chini "vizuri" alipojiangusha katika mechi ya Manchester United dhidi ya Arsenal kuhamasisha kupiga mbizi kwa mujibu wa Hiddink



Katika mechi ya Manchester United dhidi ya Arsenal wikiendi iliyopita si ushindi wa Mashetani wekundu tu na Rashford vilivyovutia wengi, ila picha ya LVG akijiangusha mbele ya mwamuzi wa nje nayo ilipata umaarufu.
Hadi sasa imeingia kwenye hariri nyingi za mitandaoni ikihusishwa kwenye vichekesho mbalimbali.
Mdachi mwenzake Guus Hiddink alivyokua kwenye mahojiano na waandishi wa habari alifunguka kuwa, kinadharia kabisa ile ilikuwa ni mbinu ya kocha wa Manchester United kuhamasisha kujiangusha.
Guus Hiddink aliendelea kusema “Nadhani unaelewa kuwa van Gaal ni mwalimu wa mazoezi tena mahiri sana, anafanya judo pia. Mimi nilikua nacheza Judo na kwa jinsi ninavyoona amejiangusha vizuri sana, hata mimi naweza fanya hivyo pia.”
Meneja huyo wa Chelsea amesema hata yeye anaweza kufanya alichofanya Van Gaal lakini si lazima niige alivyojiangusha.
Kocha wa Chelsea Guus aliwahi kuanzisha kitengo cha Judo akiwa kocha wa PSV kwao Uholanzi. “Nilianzisha kitengo cha Judo na mimi nikiwa mmoja wa wanafunzi kwa lengo la kuleta stamina kwenye timu.
"Simaanishi kwamba wachezaji walete Judo uwanjani lakini kuwa imara uwanjani ni muhimu sana ili waweze kutawala mchezo.”
Kwenye Judo kocha Hiddink alianza kuwa na mkanda mweupe ambao ni kwa ajili ya mafunzo ya awali