Taifa Stars yaanza kujipanga kwa mechi za kufuzu kushiriki AFCON 2017


 Mbawna Samatta na nahodha wa Taifa Stars, Nadir Haroub




Timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars itakuwa na kambi ya mazoezi ya siku mbili kabla ya mechi mbili mfululizo za Kundi G nyumbani na ugenini dhidi ya Chad
Taifa Stars itakuwa ikijandaa kwa ajili ya mechi za hatua ya makundi kuwania tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2017. Kocha wa Taifa Stars Charles Mkwasa ameiambia Goal, anajiandaa kutangaza kikosi ambacho atakitumia katika mechi hizo ambazo ni muhimu kwa kupata ushindi ili kuweka hai matumaini ya Tanzania kufuzu fainali hizo za mwaka 2017.
“Hizo ni mechi ngumu na hatuna muda wa kutosha kufanya maandalizi lakini nafurahi wachezaji wengi wapo kwenye viwango vizuri hivi sasa kutokana na Ligi Kuendelea naamini kila mchezaji atakaye pata nafasi atafanya kazi yake kwa asilimia 100, kulipigania taifa,”amesema Mkwasa.
Machi 25 mwaka huu, Taifa Stars itamenyana na wenyeji, Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya mjini N’Djamena katika mchezo wa Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 nchini Afrika Kusini kabla ya timu hizo kurudiana Machi 28, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam