KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amekanusha uvumi ulioenea katika mitandao ya jamii kuhusu kukamatwa magaidi mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo waliokuwa wamejitayarisha kukishambulia Chuo cha Uhasibu (Institute of Accountancy Arusha - IAA) wakidaiwa kuwa na gari aina ya Toyota Premio nyeusi ikiwa na watu wanne na bunduki nne aina ya SMG na risasi 160 walipojaribu kuingia chuoni hapo.
Inadaiwa katika taaifa hiyo isiyojulikana chanzo chake kwamba watu hao walijifanya ndugu wa mwanafunzi mmoja wa kike anayeishi kwenye hosteli zilizo ndani ya chuo hicho.
Rais wa chuo hicho, Iman Mkumbo, naye amesema habari hizo hazina ukweli wowote.
Views: 313