Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema anasubiri kukamilika kwa utaratibu wa CCM wa kugombea urais ili aingie rasmi kwenye mbio hizo kwa kuwa anaridhika na mambo matatu ambayo anasema yanamfanya ashawishike kugombea nafasi hiyo.
Msome mwenyewe mambo anayojivunia nayo...
“Niliendesha Bunge la Katiba kwa mafanikio na hata kupatikana kwa Katiba Inayopendekezwa,Watanzania wataangalia wenyewe historia yangu kwani mimi ndiye mwenyekiti niliyefanikisha kutimiza ndoto za Watanzania kupata Katiba mpya kupitia Bunge Maalumu la Katiba, haikuwa rahisi katika tukio hilo,” alisema.
“Mimi ndiye niliyebadilisha Bunge baada ya kubadilisha kanuni za Bunge mwaka 2007, ambazo zilitoa uhuru, haki na usawa kwa wabunge wote bila kujali wapinzani,” alijigamba.
“Bunge langu ndilo liliibua umaarufu wa wapinzani na ndipo wakaibuka akina Zitto Kabwe na Dk Wilbroad Slaa kwani walipata nafasi ya kuibua hoja na kuhoji udhaifu wowote wa Serikali.”
“Nilipingwa sana lakini nikasema hapana, kuna Tunu za Taifa zilizokuwa zimeharibiwa na lazima tuzirejeshe na matokeo yake kwa sasa yameanza kuonekana,” “Hata katibu mkuu wetu wa CCM, Abdurahman Kinana ambaye anakosoa Serikali na kuagiza uwajibikaji, siyo kuwaachia wapinzani tu, anayaona na anasema kwa kuwa wanaofanya hayo yanayoonekana ni watu wetu ndani ya CCM,”
“Nimefanya kazi na marais wa awamu zote, wananikubali kwa kuwa mimi ni mchapakazi. Wasingekuwa wananichukua kama si mchapa kazi,” “Katika kipindi hiki, lazima Watanzania wachuje na waangalie ni kiongozi gani atakayewafaa katika uongozi ujao na si kukurupuka na kudanganywa,” alisema.