MAGWIJI WA TANZANIA WALIVYOLALA 2-1 KWA BARCELONA


Patrick Kluivert akijaribu kuwatoka wachezaji wa Tanzania.
Shadrack Nsajigwa akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa Barca.




Kikosi cha magwiji wa Tanzania.
Kikosi cha magwiji wa Barcelona.
Kluivert akiwa amembeba mtoto Albino kabla ya mchezo kuanza.
Patashika wakati wa mechi hiyo.
TIMU ya magwiji wa Tanzania jana ilichapwa mabao 2-1 na magwiji wa Barcelona katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Taifa, jijin Dar.
Mabao ya Barcelona yaliwekwa kimiani na Luis Garcia dakika ya 9 ya mchezo na la pili likifungwa na Mholanzi, Patrick Kluivert dakika ya 86 kwa mkwaju wa penalti.
Bao la magwiji wa Tanzania lililwekwa kimiani na Yussuph Macho ‘Musso’ dakika ya 44.
VIKOSI:



Tanzania; Peter Manyika/Juma Kaseja dk46, Shadrack Nsajigwa, Abubakar Kombo, John Mwansasu/Bakari Malima dk46, Mustapha Hoza, Shaaban Ramadhan/Nico Nyagawa dk21, Nassor Mwinyi Bwanga/Deo Lucas dk31, Haruna Moshi ‘Boban’, Yussuph Macho/Salvatory Edward dk50, Bita John na Duwa Said.
Barcelona; Tito Bonayo, Mandieta, Mingo, Alber Thomas, Roger Garcia, Luis Milla, Luis Carreras, Santi Ezquerro, Patrick Kluivert, Luis Garcia na Simao Sabrosa.