Story ya Dudu Baya kukwapua Simu Bar hii hapa, --->>>Nusura Wananchi Wamchome Moto










Msanii Dudubaya Ameingia katika Skendo nyingine baada ya kushutumiwa kutaka kuiba simu ya mdau mkubwa wa Twanga pepeta ajulikanae kama Mapao ambae alikuwa amekaa naye meza moja pale Mango Garden huku Twanga Peteta wakiburudisha Tarehe 14 March..
Inasemekana Papa Mapao baada ya kutosheka na Burudani aliamka na kuondoka lakini baada ya kufika nje alishtuka kuwa ameacha simu mezani na kurudi lakini alikuta simu haipo na mtu aliyemwacha hapo ni Dudubaya ambae bado alikuwa hapa .Hali ilikuwa mbaya ukumbini kwani baadhi ya mashabiki walipendekeza Dudubaya Asachiwe lakini ghafla simu ilionekana miguuni kwa Dudubaya akiwa ameikanyagia na viatu..ilibaki kidogo jamaa wamchome Moto ..alisema mdau mmoja aliyekuwepo eneo la Tukio.....