Gazeti la Kiu Limetoa Siri kuwa Dansa wa Diamond Moses Iyobo amedaiwa kuanza kurithi mali za mume wa Msanii Aunty Ezekiel, Sunday Demonte Ambaye yupo Gerezani nchini Abu Dhabi akitumikia kifungo cha Miaka Kumi .
Mali anazodaiwa kurithi Iyobo ni pamoja na nguo anazodaiwa kuonekana nazo mitaani na kwenye Show za Diamond..Chanzo cha ndani kinasema nguo hizo ni zile alizokwenda kuzichukua Aunty ezekiel nyumbani kwake nchini Dubai siku chache baada ya Demonte kusekwa Jela..
"Kuna uwezekano Iyobo hajui kama nguo hizo ni za Demonte lakini ukweli ndio huo, nguo hizo sisi tunazijua na Demonte alikuwa akizivaa sana Dubai sasa tunashangaa mtu hajafa nguo zake zimesharithishwa kwa mwanaume mwingine" Kililalamika Chanzo cha habari hii
Aunty Ezekile alipotafutwa kuzungumzia hilo Simu yake iliita bila Kupokelewa...