Nyalandu: Urais Mwaka Huu ni Kivumbi ila Simuogopi Mtu Kati ya Wote Wanaotajwa






Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema uchaguzi wa Rais ajaye utakuwa na ushindani mkubwa ndani na nje ya CCM, huku akibainisha kuwa haogopi mtu kati ya wote wanaotajwa kwenye kinyang’anyiro hicho, bali anawaheshimu.

Lakini mbunge huyo wa Singida Kaskazini amesema mgombea pekee atakayemwogopa ni yule atakayekuwa anataka kulipiza kisasi dhidi ya wagombea wengine.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo jana wakati alipofanya ziara kwenye makao makuu ya Ofisi za Mwananchi Communications inayozalisha magazeti ya The Citizen, Mwananchi na Mwanaspoti zilizoko Tabata Relini kando ya Barabara ya Mandela.