Akizungumzia Hekaheka ambayo iliwahi kukutana nayo kuna siku walienda Shinyanga kwenye michezo ya jadi kitaifa, akakutana na dada mmoja ambae alitaka kufanya filamu wakawa wanawasiliana.
Baadaye mume wa dada huyo alimtuhumu Muhogo kuwa na uhusiano na mpenzi wake baada ya kukuta message walizokuwa wanatumiana, japo alijaibu kumuelekea kuwa walikuwa kwenye majadiliano kuhusu filamu mwanaume huyo hakuelewa.
Kuhusu watu ambao anapenda kucheza nao filamu amesema anaelewana sana na Bi Staa kutokana na kwamba walianza wote sanaa.
Muhogo Mchungu amesema anaipenda sana tamthilia ya Fukuto na filamu ya Kigodoro.