Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, akiwa na mume wake, Emmanuel Mbasha.
KESI ya kudaiwa kumbaka shemeji yake inayomkabili mfanyabiashara na mwimba Injili Bongo, Emmanuel Mbasha imeendelea kuunguruma leo katika Mahakama ya Ilala jijini Dar ambapo mkewe Flora alifika na kutoa ushahidi kwa siri.
Siku hiyo, shahidi namba nne ambaye ni daktari anatarajiwa kutoa ushahidi wake na mshitakiwa anaendelea kuwa nje kwa dhamana. Mbasha anashtakiwa kwa makosa mawili ya ubakaji, la kwanza anadaiwa kulifanya Mei 23, mwaka jana, eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam na Mei 25, mwaka jana akidaiwa kutenda kosa hilo kwa binti huyo kwa mara nyingine eneo hilohilo.