VURUGU IRINGA, WANANCHI WAFUNGA BARABARA KUU----->>>





Muonekano wa mji wa Ilula mkoani Iringa baada ya wananchi kufunga barabara kuu ya mji huo.
Mabasi ya kwenda mikoani yakiwa yamepaki baada ya wananchi kufunga barabara.
WANANCHI wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa,  wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo asubuhi kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.
Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita,  hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.
Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.
Hadi tunakwenda mitamboni, habari zinasema wananchi kadhaa wamejeruhiwa katika kadhia hiyo.