TAZAMA KILICHOJIRI LEO KESI YA HALIMA MDEE NA WENZAKE!!!.........






Mwenyekiti wa BAWACHA, Halima Mdee (mwenye nguo nyekundu) akitoka mahakamani.



...Akisalimiana na Ofisa wa Oparesheni wa Kinondoni, Emmanuel Tille (mwenye tai) ambaye ni shahidi upande wa jeshi la polisi.
KESI inayowakabili wanachama tisa wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwemo wanawake wanane wa Baraza la Wanawake Chadema  (BAWACHA)  na mwanaume mmoja, leo imeahirishwa  na itaendelea kesho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Watu hao ambao ni pamoja na Mwenyekiti wa BAWACHA, Halima Mdee, wanakabiliwa na kesi ya kukiuka amri ya jeshi la polisi iliyowataka wasiandamane  4 Oktoba 2014  katika dhamira  ya kupinga katiba iliyopitishwa na  bunge la katiba.