Polisi wa Ufaransa wametoa majina na picha ya washukiwa wawili waliohusika na shambulio katika ofisi za jarida la vibonzo nchini humo.
Polisi wamemtaja Said Kouachi na kaka yake Cherif wanaweza kuwa watu hatari na wenye silaha.
Cherif Kouachi aliwahi pia na kuhusika na kupeleka wapiganaji wenye msimamo mkali wa kidini nchini Iraq.
Vyombo vya Habari vya Ufaransa vimesema mtu wa tatu ambaye amegunduliwa pia kama ni mshukiwa Hamyd Mourad mwenye umri wa miaka 18 alijisalimisha polisi baada ya kuona jila lake katika mitandao ya kijamii.
Baadhi ya rafiki zake walisema katika mitandao hiyo kwamba alikuwa shule wakati shambulio hilo katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo likitokea, ambako watu 12 waliuawa.
Uchunguzi mkali bado unaendelea kuwasaka watu hao wenye silaha.
Awali jarida hilo lilipandisha hasira kwa waislamu baada ya kuchapisha kibonzo walichodai kuwa ni Mtume Muhamad SAW