DOCTA DRE ASHITAKIWA

Dr Dre akivalia vipaza sauti vya beat
Wasanii mashuhuri wa Marekani Dr Dre na Jimmy Loving wanashtakiwa na mshirika wao wa kibiashara ambaye waliunda naye vipaza sauti vya masikioni ama headphones kwa jina Beats Headphone range.
Noel Lee ambaye kampuni yake Monster ilisaidia kuzindua vipaza sauti hivyo vya Dr.Dre mnamo mwaka 2008,anasema kuwa kampuni yake ilisalitiwa na teknologia yake kuibwa.
Dr Dre
Anadai kwamba alipoteza mamilioni baada ya msanii Dre na Jimmy Iovine walithibiti visivyo vipaza sauti hivyo kupitia udanganyifu.
Baada ya kukata uhusiano wake na Monster,Beats ilinunuliwa na Apple kwa dola billioni 3.
Katika nakala za kesi hiyo zilizowasilishwa katika mahakama ya Carlifonia,Lee anadai msanii huyo wa muziki wa rap Dr Dre hakuhusika pakubwa katika kutengeza vipaza sauti hivyo vilivyo na jina lake.
Dr Dre na wenzake
Lakini vipaza sauti hivyo vilipata umaarufu mkubwa na kuanza kutumiwa na watu mashuhuri na mashabiki wa muziki huku ushawishi wa Dr Dre ukifanya biashara hiyo kufaulu.
Wakati kmapuni hiyo ilipouzwa kwa kampuni ya simu ya HTC mnamo mwaka wa 2012,Dre na Loving walitia kibindoni kitita cha dola millioni 100 kila mmoja wao.
Hakuna tamko lolote kutoka kwa wakili wa Dr Dre ama kutoka kwa beats.