HABARI NJEMA JIJINI LEO-MABEHEWA MAPYA YAWASILI NCHINI,SASA TRL KUWA YA KISASA-SOMA HAPA KUJUA


Pichani ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka akikagua mabehewa mapya leo jijin Dar es Salaam
NA Karoli Vinsent
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imedhamilia kuliboresha Shirika la Reli ya kati TRL ili liweze kujiendesha lenyewe na kuacha kutegemea bajeti ya Serikali kwenye mipango yak,baada ya leo kampuni hiyo imepokea Mabehewa 50 ya kubebea makasha (Containres), ikiwa ni sehemu ya mradi wa serikali wa ununuzi wa mabehewa mapya 274 kutoka nchini India.
Kupokelewa kwa mabehewa hayo, kunatarajia kuongeza kasi ya utoaji wa makasha ya mizigo kutoka  Bandari ya Dar es Salaam kwa njia ya reli kwenda nchi jirani za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda na kutimiza malengo ya Big result yaani matokea makubwa sasa.
       Akipokea Mabehewa hayo leo Kwenye bandari ya Jijini Dar es Salaa na kushuhudiwa na waandishi wa habari pamoja v, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka, alisema  serikali inaendelea kutekeleza miradi 12 kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN), yenye lengo la kuimarisha huduma ya usafirishaji kwa njia ya reli.
Hapa ndipo Mahebewa hayo yakiwasili leo Jijin Dar es Salaam kwenye bandari
Alisema serikali imeshalipa zaidi ya bilioni 45 ikiwa ni gharama za ununuzi wa mabehewa 274 ambayo ni wastani wa milioni 166 kwa kila behewa.
        Vilevile Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa , lengo la serikali ni kuiwezesha TRL kusafirisha mizigo tani milioni 1.5 kwa mwaka na kuiwezesha kampuni hiyo kujiendesha kwa faida.
Vilevile akatabainisha kuwa, baada ya kukamilika kwa mradi huo kutapunguza uharibifu wa barabara kutokana na mizigo mingi kusafirishwa kwa njia ya barabara.