Happiness
Watimanywa (20) aliyekuwa Redds Miss Tanzania 2013 sasa yuko jijini
London Uingereza kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya
Miss World 2014.
Happiness
ambaye kwa sasa anashikilia taji la Miss World Tanzania 2014 amesema ana
kila sababu ya kurudisha taji nyumbani ikiwa watanzania watamuunga
mkono kwa kusambaza video zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
"Hebu
angalia uzuri wa taifa letu, amani, upendo na vivutio mbalimbali vya
utalii. Hebu niangalie na mimi mwenyewe... tuna kila sababu ya kurudisha
taji nyumbani." alisema Happiness Watimanywa
Shime shime watanzania, tumuunge mkono wa nyumbani kwa ku-retweet, ku-like na ku-share post zake mbalimbali kwa kutumia Hashtag #Happiness4MissWorld