UPDATES SAKATA LA ESCROW HIZI HAPA!...

Twitter account ya JamiiForums wana updates Mvutano unao endelea kuhusu kusomwa au kutokusomwa Kwa Ripoti ya Escrow. Fuatilia twitter Acount ya jamiiforums Kupitia JamiiForums



*Yabainika: Serikali imesisitiza amri ya Mahakama itekelezwe ili #TegetaEscrow report isisomwe Bungeni

*UPDATE: Serikali (Lukuvi na wenzie) wanadaiwa kutumia mabavu #TegetaEscrow Report isomwe tu bila kujadiliwa!

*UPDATE: Watu wa PAP na hati yao ya mahakama wapo getini Bungeni wakitaka kutoa hati kwa BUNGE. BUNGE limegoma kupokea! #TegetaEscrow

*UPDATE: Spika & Katibu wa Bunge wamejifungia ofisini kwa spika kujadili kabla ya Kamati ya Uongozi. Wenyeviti wengi
hawajafika #TegetaEscrow

*UPDATE: Wenyeviti Waliofika mpaka sasa ni Ngwilizi, Msola, Mbowe na Serukamba #TegetaEscrow

*UPDATE: Wabunge wamepewa nyaraka bila hata kuwasilisha kwa kusoma. Kamati ya Uongozi inajadili amri ya mahakama! #TegetaEscrow

*UPDATE: Taarifa za sasa zinabainisha Bunge litaahirishwa hadi jioni! #TegetaEscrow

*UPDATE: Hati hii ndo imeleta kasheshe Bungeni na kupelekea #TegetaEscrow report kuwa kaa la moto!


*UPDATE: Katika Kikao cha CCM jana usiku, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mangula alitaka wahusika wajiuzulu, wao hawataki! #TegetaEscrow

*UPDATE: Bunge limekataa kupokea order ya mahakama. Ripoti ya PAC itasomwa jioni na si asubuhi tena #TegetaEscrow

*UPDATE: Katika kikao cha jana usiku cha CCM; Muhongo alitoa maelezo kwamba pesa si za umma na kwamba taratibu zilifuatwa #TegetaEscrow

*
TIP: Kuna mgawanyiko ndani CCM juu ya #TegetaEscrow; Mizengo Pinda anatakiwa abaki Mawaziri na watendaji waliohusika wang'oke!
CREDIT: Jamiiforums.com