Meneja wa Skylight Band Aneth
Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa
iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku
akisindikizwa na waimbaji wenzake kutoka kushoto ni Digna Mbepera,
Joniko Flower a.k.a Baba lao, Sony Masamba pamoja na Sam Mapenzi.
Aneth Kushaba sambamba na Digna
Mbepera wakiwapa raha mashabiki wao (hawapo pichani) kwenye show zao za
kila Ijumaa ndani ya ukumbi wa maraha wa Thai Village Masaki jijini Dar.
Kifaa kipya cha Skylight Band
Bela Kombo akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo ndani ya ukumbi
wa Thai Village Ijumaa iliyopita.
Kutoka kushoto Bela Kombo, Hashim
Donode na Digna Mbepera wakiporomosha burudani kwa mashabiki wa
Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya uwanja wao wa nyumbani Thai
Village.
Binti mwenye sauti ya kumtoa
nyoka pangoni Digna Mbepera kwenye hisia kali za muziki wa Live kwa
mashabiki wa Skylight Band ndani ya ukumbi wa Thai Village Masaki jijini
Dar.
Burudani ikiendelea.
Mashabiki wa Skylight Band
wakiburudika na muziki safi kabisa wa ladha na vionjo vya kila aina
ikiwemo Reggae, Kwaito, Naija Flava, R&B, Zouk na zingine kibao bila
kusahau sebene pale kati Joniko Flower anahusika sana sambamba na Sony
Masamba njoo ufunge mwezi Oktoba na Skylight Band usiku wa leo.
Anaitwa Sony Masamba akifanya yake jukwaani huku Sam Mapenzi na Joniko Flower wakipiga back vocal.
Oya shake body....Oya move
body....Make you ring alarm o....Oya shake body....si mwingine ni Sam
Mapenzi na Naija Flava njoo leo umshuhudie kwa macho yako...Skylight
Band ndio kila kitu huna haja ya kwenda disco unapata kila kitu hapa
hapa...!
Aaaah ni full raha wake kwa waume
wakionekana kukunwa na uimbaji wa Sam Mapenzi mzee wa Naija Flava,
unakosaje uhondo ndugu....Njoo tujumuike leo pamoja ndani ya Thai
Village.
Umati wa mashabiki wa Skylight Band wakiyarudi mangoma ya ukweli yaliyoenda shule, tukutane pale kati kuanzia saa tatu usiku.
Mpiga drum wa Skylight Band
Baraka akifanya yake kuhakikisha mashabiki wanapata ladha nzuri ya ala
hizo za muziki huku pale pembeni Amos Kinanda naye akisababisha.
Na hivi basi ndivyo
wanavyochizika mashabiki wa Skylight Band kwa shangwe za aina yake
mwenye kigelegele haya...mwenye mluzi haya....ni furaha si kingine.
Mkongwe wa muziki Joniko Flower
akiwasebenesha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota
cha Thai Village Masaki jijini Dar huku waimbaji wenzake wakimpa sapoti.
Sam Mapenzi;……Kuna Watu Hatari, Wenye Mapenzi Zenye Siri Kali,…Letu Nalo Lina Jua Kali, Penzi Letu Serikali,….Wajua Nakupenda, Malaika…..Aneth Kushaba;…..I'm
Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I, Love You, (Aiyayaaaaa)….I'm
Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I Love You,….(Aiyayaaaaa)...Hizi
zote utazipata Skylight Band si kwingine bonge la colabo.
Nyomi la mashabiki wa ukweli wa Skylight Band likiwa limefurika Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village.
Supermodel Neema Mbuya akionyesha upendo kwa mpiga picha na busu bashasha....Santeeee!
We are twin sisters......!
Blogger King Kif (kushoto) akiwa na wadau wa Skylight Band ndani ya ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar.
Meneja Maneno na King Kif wakimezea mate kuku choma ndani ya kiota cha Thai Village Masaki.