Helkopta aina ya Chopa iliyoanguka maeneo ya Kipunguni B Ukonga jijini
Dar es Salaam, leo asubuhi na kuua watu wanne waliokuwemo akiwa ni
rubani pamoja na askari watatu.
Miili ya watu waliokuwemo kwenye helkopta hiyo ikiwa imekandamizwa na mabaki ya chopa hiyo.
Helkopta inayosemekana inamilikiwa na TANAPA imeanguka na kuteketea kwa
moto katika eneo la Kipunguni B Ukonga jijini Dar es Salaam leo
asubuhi.
Kwa mujibu wa mashuhuda, wamesema waliona helkopta hiyo ikipoteza
uelekeo na badaye kuanguka chini hali iliyosababisha kishindo kikubwa
baada ya kulipuka moto.
Inasemekana ndani ya helkopta hiyo kulikuwa na watu wanne ambao wote
wameripotiwa kufariki dunia.Aidha imeelezwa kuwa katika ajali hiyo
kulikuwamo na Askari 3 na rubani. Picha kwa hisani ya Sufiani Mafoto