Wananchi chukueni hatua za dharura!!!

====UPDATES====
- Tayari walioiba ripoti hiyo washaanza kukamatwa. Mohamed Mbaruk ndugu wa Prof. Muhongo amekamatwa na shehena ya ripoti hiyo iliyonyofolewa kurasa 56,57,59... Kwa sasa yupo kituo cha Polisi kati Dodoma na amewataja walio kwenye zoezi la kusambaza ripoti hiyo kuwa ni pamoja na mtu maarufu aitwae "Chifu Kiumbe" ambaye Jeshi la Polisi tayari wanamfuatilia kwa ukaribu usiku huu. Na mwisho amesema katumwa na wakubwa (mafisadi).



Taarifa ya (CAG) yakutwa ikisambazwa mitaani ikiwa imenyofolewa kurasa.
Taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali kuhusiana na kashfa ya wizi wa bilioni 321 kwenye akaunti ya tegeta Escrow iliyokabidhiwa kwa katibu wa bunge imekutwa inasambazwa mitaani huku ikiwa imenyofolewa kurasa tatu za mwisho zenye majina ya waliohusika na mgawo wa fedha hizo kwa lengo la kutengeneza propaganda ili kuwadanganya wananchi kuwa taarifa hizo hazijawataja wahusika.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti mwenza wa ukawa Mh. James Mbatia amesema zipo taarifa za baadhi ya waliokuwa wanasambaza taarifa hizo kuwa wamekamatwa na jeshi la polisi na kuwataka wananchi kutoa taarifa kituo cha polisi ili waweze kuchukuliwa hatua haraka ambapo amesesistiza kwamba (UKAWA) wanataka taarifa hiyo iwasilishwe bungeni kwa ajili ya kujadiliwa Jumatatu .

ITV imemtafuta kamanda wa polisi mkoa wa dodoma David Misime na katibu wa bunge Dr.Thomas Kashilillah ambao wamesema nao wanazisikia taarifa hizo na wanazifanyia kazi ili kutoa taarifa yao.

Chanzo: ITV