Duh hatari kweli kweli
Hivi inakuwaje mtu anafikia hatu akama hii jamani chuki gani hizi??? Damnnnnnnnn!!!!!
“Kiukweli
mimi kama Jacquline Wolper sina ubaya na mtu yeyote, ila nmeshangaa
kuona watu nisiyo wajua kuja usiku wa manane na kunichomea gari yangu.
Kiukweli siwezi kumuhisi mtu ila najua ni lazima atakua mtu asiependa
maendeleo yangu ni ni mtu mbaya sana kwangu. Na inawezekana kabisa
alipanga kunia lakni kwa bahati nzuri siku hiyo sikua nyumbani nilikua
nimesafiri. Tukio lilitokea usiku wa tarehe 23/10/2012 ambapo mtu
alitumia matambara yaliyo na mafuta ya taa au Petrol akiwa kwa nje ya
ukuta wa nyumba yangu akiwa anarusha kwa ndani. Nimepeleka taarifa kituo
cha Polisi kawe kwa kutaka msaada wa kiupelezi na nitakua nawapa
taarifa za kila kinachoendelea. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwani niko
salama” Alisema Wolper
Pole sana Jacqueline and take care. Nadhani anahitaji security ya uhakika kabla mambo hayajawa mengine. Inasikitisha sana
Culled from This is Diamond