Irene Neema Vedastous 'La Veda', Mshiriki wa Big Brother Hotshots kutoka Tanzania.
IRENE NEEMA
VEDASTOUS ni msichana mrembo wa Kitanzania, mwenye umri wa miaka 23
anayeiwakilisha Tanzania katika shindano la BIG BROTHER 2014 ‘HOTSHOTS’
nchini Afrika Kusini
La Veda katika pozi na baadhi ya mastaa.
Mrembo huyu
ambaye ameshawahi kuingia 10 bora ya shindano la Miss Tanzania mwaka
2012, baada ya kutwaa taji la Miss Lindi 2012, anaingia rasmi leo tarehe
5 Oktoba 2014 kwenye shindano hilo lenye mashabiki wengi duniani ambalo kuanzia saa 1 jioni litakua likirushwa live kupitia DSTV kwenye channel namba. 198.
Irene Neema Vedastous aka Irene La Veda ni nani?
Irene La Veda, sio mrembo mpya kwenye jamii ya Watanzania kama wengi wanavyodhani, ni mrembo anayependa kujichanganya na watu mbalimbali. Hii hali imemuwezesha kufanya vitu mbalimbali na
vikubwa kwenye fani mbalimbali kama filamu, muziki, urembo, mitindo, nk.
La Veda akiwa kazini.
MUZIKI:
Kwa upande wa muziki, La Veda ni mkali sana wa kucheza na tarumbeta.
Hii ni nadra sana kukutana na mwanamuziki ambaye anauwezo wa kupiga
kifaa japo kimoja cha muziki.Mrembo La Veda sio tu mkali wa kupuliza tarumbeta bali ameshatoa vibao mbalimbali kama UTANIMISS, SIMPLE LOVE, LET IT GO, na kibao kikali kinachotamba kwenye mitandao mbalimbali, kibao
ambacho kinaitangaza Tanzania katika sekta ya utalii kiitwacho TWENDE TUKATALII , Video ya wimbo huu inapatikana You tube.
La Veda (wa kwanza kulia) akiwa na baadhi ya washiriki wa Miss Tanzania 2012.
UCHEZAJI DANSI: Mshiriki huyo ni dansa mzuri na umahiri wake tayari ameuonyesha katika video zake alizofanya pamoja na kazi nyingine za muziki alizofanya hapa Tanzania na nje ya nchi zikiwemo Uswiss na Ufaransa.
MITINDO NA UREMBO: Licha ya kuwa Miss Lindi 2012, La Veda ni mwanamitindo ambaye tayari ameshafanya 'events' mbalimbali za mitindo mojawapo ikienda kwa jina LA VEDA SHOW.
Irene La Veda ambaye hasiti kusema 'Role Model' wake ni Mama yake Mzazi, moja ya mipango yake ni kuona anafika mbali kisanaa, hivyo aliamua kwenda kukaa darasani kwenye Chuo Cha Sanaa
Bagamoyo mwaka 2012 kuongeza ujuzi na utaalamu katika fani hiyo.
Mama Mzazi wa La Veda, Mecky Sebastian anasemaje kuhusu mwanaye kushiriki Big Brother Hotshots? msikie hapa; "Naomba akina mama wenzangu, wasanii na Watanzania wote kwa ujumla mnisaidie katika kumuunga mkono La Veda ili aweze kuiletea heshima nchi yetu na yeyote popote alipo mwenye kuitakia mema
Tanzania na Afrika Mashariki tumpe ‘support’ ya kutosha ili aweze kuibuka mshindi. Nawatakia Watanzania kila la kheri kwenye shughuli zao za maendeleo", alisema Mama Mzazi wa La Veda, Mecky
Sebastian.


