Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo,juu ya onyesho la Redd's Miss Tanzania 2014 linalotarajiwa kufanyika Oktoba 11, 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar. Katikati ni Meneja wa Kinywaji cha Redd's ambao ni Wadhamini Wakuu wa Mashindano hayo,Victoria Kimaro na kushoto ni Meneja Maria Stopes Tanzania,Anna Shanalingigwa.
Sehemu ya Wanahabari pamoja na Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014 wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga alipokuwa akizungumza.
Sehemu ya Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014







