Halima Mdee na wenzake wakitoka mahakamani baada ya kuachiwa huru kwa dhamana leo.
Halima akiwa na wanachama wa Chadema baada ya kuachiwa huru.
Halima akiwa na wanachama wa Chadema baada ya kuachiwa huru.
Mdee akiwa juu ya gari akitoka nje ya mahakama.
Wafuasi wa Chadema wakionyesha bango lenye ujumbe wa kumpongeza mbunge wao.
Gari la wanachama wa Chadema likitoka katika mahakama.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wenzake 8 leo wamepata dhamana katika Mahakama ya Kisutu, Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014.
Siku ya jana washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Kaluyenda na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu, Kangola aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi, Penina Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari.
Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf iliyowataka watawanyike.
Shtaka la pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika kinyume na sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais.
(Habari/Picha na: Deogratius Mongela na Denis Mtima/GPL)