Mabingwa wa shindano la Dance 100% 2014” WAKALI SISI”wakimsikiliza kwa makini Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia) wakati alipokuwa akiwahusia kuhusiana na matumizi mazuri ya simu baada ya kuwakabidhi rasmi ya simu zao aina ya Vodafone Smart Kicka zilizounganishwa na Vodacom na muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi laki moja ambazo ni moja ya zawadi walizojishindia katika fainali ya shindano hilo na kuibuka washindi wa kwanza na kujizolea kombe pamoja na kitita cha shilingi milioni 5.
Kiongozi wa kundi la”WAKALI SISI” la Kiwalani jijini Dar es Salaam,Baraka Kambona(kushoto) akipokea mfuko wenye simu aina ya Vodafone Smart Kicka zilizounganishwa na mtandao huo na kuwekewa muda wa maogezi wa shilingi laki moja toka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ikiwa ni kati ya zawadi walizojishindia katika fainali ya shindano la Dance 100% hivi karibuni na kuondoka na kitita cha Tsh Milioni 5.
Mabingwa wa Dance 100% 2014”WAKALI SISI”wa Kiwalani jijini Dar es Salaam,wakionesha simu aina ya Vodafone Smart Kicka zikiwa na muda wa maongezi wa shilingi laki moja mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kulia)kundi hilo liliibuka mshindi wa kwanza katika fainali ya shindano hilo hivi karibuni ambapo walijinyakulia kitita cha shilingi milioni 5
Mabingwa wa Dance 100% 2014”WAKALI SISI”wa Kiwalani jijini Dar es Salaam,wakionesha simu aina ya Vodafone Smart Kicka zikiwa na muda wa maongezi wa shilingi laki moja mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kulia)kundi hilo liliibuka mshindi wa kwanza katika fainali ya shindano hilo hivi karibuni ambapo walijinyakulia kitita cha shilingi milioni 5.
Kundi
la”WAKALI SISI”ambalo ni mabingwa wa shindano la Dance 100% 2014
wakionesha makali yao ya kucheza dansi katika makao makuu ya Vodacom
walipofika kwenye hafla fupi yakukabidhiwa simu zao aina ya Vodafone
Smart Kicka zilizounganishwa na muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi
laki moja ambazo ni moja ya zawadi walizojishindia katika fainali ya
shindano hilo na kuibuka washindi wa kwanza na kujizolea kombe pamoja na
kitita cha shilingi milioni5.
-------------------
Kundi la
”Wakali Sisi” lenye makazi yake Kiwalani jijini Dar es Salaam, ambalo
liliibuka na ushindi miongoni mwa makundi matano yaliyoingia fainali za
shindano la kucheza muziki maarufu kama Dance 100% na kujishindia kitita
cha shilingi milioni 5 wiki iliyopita leo/ jana wasanii wa kikundi
hicho walikabidhiwa simu aina ya smart Phone na kampuni ya mawasiliano
ya Vodacom.
Akiongea
katika hafla ya kuwakabidhi zawadi ya simu Meneja Uhusiano wa Umma wa
Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu,alisema kuwa kwa kushinda mashindano
hayo wamedhihirisha kuwa wana kipaji kikubwa na aliwataka wasibweteke
bali wajiendeleze ili waweze kupata mafanikio zaidi.
“Vodacom
tunaamini kuwa sanaa na michezo inaweza kutoa ajira kwa vijana ndio
maana tumekuwa tukidhamini michezo na sanaa hivyo tumia vizuri pesa
mlizopata na simu hizi tulizowazawadia kutafuta fursa za kusonga mbele
na kupata mafanikio zaidi nasi tutazidi kuwaunga mkono”Alisema Nkurlu.
Naye msemaji
wa kundi hilo Baraka Kambona aliishukuru kampuni hiyo kwa zawadi hizo
za simu na kuongeza kuwa mashindano hayo yamewafumbua macho na
wameweza kujulikana na kuahidi kuendelea na mazoezi na ubunifu zaidi ili
kundi lao lizidi kutamba katika ushindani mkubwa wa sanaa ya muziki
kwani hata jana tulitumbuiza kwenye shindano la Miss Tanzania.
Shindano hilo
linaloratibiwa na Kituo cha East Africa Television na kudhaminiwa na
Vodacom Tanzania, lilikuwa la kukata na shoka kwa ushindani mkali na
lilifikia tamati Oktoba nne katika Viwanja vya Don Bosco, Oysterbay
jijini Dar es Salaam.
Makundi
matatu yalifanikiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali katika hatua ya
fainali hiyo na vijana walikuwa wakionesha vipaji na umahiri mkubwa wa
kucheza staili mbalimbali za muziki ambayo ni Wakali sisi walioibuka
kidedea na kujinyakulia kitita cha Sh5 Milioni huku kila mshiriki katika
katika kundi hilo akipatiwa simu aina ya Vodafone Smart Kick ikiwa na
muda wa maongezi wa Sh 100,000. Mshindi wa pili ni kundi la The W.T.
ambalo lilijinyakulia Sh1.5 Milioni na mshindi wa tatu ni kundi la
Wazawa Crew lilijinyakulia Sh500,000.





