Staa mkongwe kwenye sinema za Bongo, Illuminata Poshi ‘Dotnata’ akiingizwa kwenye gari la wagonjwa.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili juzi kuwa, Dotnata aliteleza bafuni nyumbani kwake River Side jijini Dar na muda huohuo pacha wake huyo akivamiwa na majambazi na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili.
….Akishushwa kutoka kwenye gari kuingizwa hospitalini.
Baada ya kupata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Dotnata kwa njia ya simu ambapo alikuwa na haya:
Pacha wa Dotnata akiwa amevimba uso.
“Ni kweli niliteleza bafuni na kuanguka. Ni Jumamosi iliyopita, saa kumi jioni. Nimeumia, mfupa wa kwenye paja umevunjika hivyo bado niko Hospitali ya Taifa Muhimbili kwenye kitengo cha mifupa na mishipa ya fahamu (Moi). Jumanne ijayo (juzi) nitafanyiwa operesheni.“Wakati naanguka, pacha wangu naye alivamiwa na majambazi, wakamjeruhi sehemu mbalimbali za mwili. Alikimbizwa Hospitali ya Hindu Mandal lakini yeye ameshatoka, anaendelea vizuri kidogo,” alisema Dotnata.