Meninah La Diva Awatamani Wema Sepetu na Kajala..Kama Angekuwa na Uwezo Asema Angefanya Hivi.--->>





Mrembo na Staa wa Bongo Fleva, ambae nyota na jina lake lilianza kusikika Kupitia shindano la Bongo Star Search (BSS), Meninah La Diva amesema angekuwa na uwezo angewapatanisha mastaa wawili wa Bongo Movies , Wema Sepetu na Kajala Masanja ambao alisema kuwa anawependa sana.

Meninah aliyasema hayo leo alipokuwa akifanya mahojiano na mtangazaji Millard Ayo kwenye c kipindi cha Amplifaya, alipoulizwa kuwa angekuwa na uwezo angewapatanisha mastaa gani ambao wamegombana au hawaelewani kwa namna moja au nyingine.

“Ningekuwa na uwezo ningewapatatinisha Wema na Kajala kwasababu wote nawapenda”-Meninah alijibu

Wema na Kajala walikuwa marafiki wa karibu lakini urafiki wao ulivunjika na kwasasa sio marafiki tena.

Hakika wengi tunapenda wawili hawa waelewane na urafiki  wao urudi, wewe je?