Lucy Komba: Tuna Zamu ya Kupika na Mume Wangu






Mkongwe wa sinema za Kibongo ambaye amekita makazi yake nchini Denmark , Lucy Komba ameweka bayana kuwa katika suala la mapishi anapokuwa nyumbani, huwa wanawekeana zamu ya kupika na mumewe.
Lucy Komba akiwa katika pozi na mumewe .



Lucy alivujisha taarifa hiyo baada ya mwanahabari wetu kumuuliza juu ya ratiba zake za mapishi anapokuwa nyumbani ndipo alifunguka :
“Huwa tunawekeana zamu ya kupika na mume wangu, mfano kama leo , mimi nipo nyumbani lakini sipiki namsubiri atoke kwenye mihangaiko yake aje apike , huku ndivyo mambo yanavyokwenda tofauti kidogo na huko nyumbani (Bongo ) kwamba mwanamke pekee ndiye mwenye jukumu la kupika.”