STEVE Ajutia Maamuzi Yake ya Kuhamia Kuishabikia AZAM Kutoka YANGA, Asema Maisha Yake Yamekuwa Mabovu..Abembeleza Kazi Azam






Aliyekuwa mshabiki maarufu wa Team ya Yanga Steve Amefunguka na kusema kitendo chake cha kuhamia kuwa mshabiki wa Azam kutoka Yanga kimefanya maisha yake yawe Mabovu kimaslahi na umaarufu kupungua sana





Amesema japo bado anaitamani Yanga lakini hawezi kurudi tena kuishabikia Yanga kwa kutoonekana Msaliti ...Hivyo anachofanya kwa sasa ni kumuomba Bosi wa Azam Ampe kazi ya Kuajiriwa katika Team hiyo kama Mshabiki wa Damu ..

Steve alipata umaarufu mkubwa baada ya Yanga kufungwa Tano na Simba miaka kadhaa iliyopita ambapo Steve alirekodiwa na Vituo mbali mbali vya TV akimwaga Kilio cha nguvu