KAMANDA MPINGA AWAKEMEA MADEREVA WAZEMBE


Kamanda Mpinga akitoa ufafanuzi juu ya matukio yanayosababishwa na uzembe wa madereva.



/L5FNdOkpk1aXo*4LP0TgORGZ0tdFmmdDxhkvlJKAVjUv7tSJdcWbP04HCtEsUS4o7y2dy4ghi30lKDKHsyxd5P11CoE01-5U/2.Sehemuyawanahabari..JPG" target="_self">Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakimsikiliza Kamanda Mpinga (hayupo pichani).
Kamanda Mpinga akisikiliza swali kutoka kwa mmoja wa wanahabari (hayupo pichani).
KAMANDA wa Kikosi  cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga ametoa tamko kuhusiana na madereva wote waliosababisha ajali kwa uzembe kuwa watafutiwa leseni zao mara moja.



Akizungumza na wanahabari leo mchana katika Ofisi za Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar, Kamanda Mpinga alisema kuwa katika kukabiliana na wimbi la ajali, wamedhamiria kufuta leseni zote za madereva wazembe ili kukomesha ajali zinazoendelea kutokea nchini.
Kamanda Mpinga alisema hivi karibuni kumetokea ajali ambazo miongoni mwa ajali hizo zimesababishwa na uzembe wa madereva hivyo ni dhahiri kuwa lazima madereva waliohusika kufanya uzembe wafutiwe leseni ili wasiweze kufanya kazi sehemu yoyote ambapo wote wataofutiwa leseni zao, watawaanika katika tovuti mbalimbali ili iwe fundisho kwa wengine.
Alisema kwa upande wa mabasi yanayosafirisha abiria kutoka sehemu moja kwenda nyingine, Kikosi cha Usalama Barabarani kitahakikisha kinazingatia muda uliopangwa wa kufika kituo husika na endapo dereva atakiuka kwa kutozingatia muda atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha, Mpinga alitoa rai kwa wananchi wote wanaosafiri katika vyombo vya usafiri kutoa taarifa mara moja pale wanapoona dereva anakwenda mwendo kasi usiozingatia sheria za usalama barabarani.
Mwishoni, Kamanda Mpinga alitoa salamu za pole kwa ndugu jamaa na marafiki walioguswa na vifo 103 vilivyotokea kwa kipindi cha Machi mwishoni hadi sasa na kuwataka wafiwa kuwa na moyo wa subira katika kipindi hicho kigumu.
credit: GPL