moyo, wakiongozwa na hasimu wake wa karibu, Kajala Masanja, ambaye amesema hana sababu ya kukata tamaa, kwani bado ni mdogo.
Akizungumza na na gazeti la Risasi Mchanganyiko baada ya kuombwa maoni yake, Kajala alielezea masikitiko yake juu ya hali ya rafiki yake wa zamani, lakini akasema anaamini hana tatizo kubwa la kumfanya asipate kabisa mtoto, isipokuwa anadhani bado hayampata mtaalamu sahihi wa masuala ya wanawake anayeweza kumsaidia tatizo alilonalo.
“Namuombea sana kwa Mungu, lakini sitaki kabisa kuamini kama hawezi kupata mtoto katika maisha yake, mbona bado kijana sana, atapata tu bwana,” alisema Kajala, ambaye ana mtoto aitwaye Paula.“Sitaki kuamini, roho inaniuma sana, namshauri Wema asiumie wala kuwa mnyonge. Na watu waache kumuumiza kwa maneno ya kebehi, lakini kama Wema akiwa tayari kulea mtoto wa mwenzake, anione, nina imani atapata mtoto atamlea na kumtunza kama wake.
“Naomba achukue mfano wangu mimi Wastara, Mungu kanipokonya mguu kanipa watoto, natumia mguu wa bandia na ninatembea lakini Wema amepewa kila kitu kasoro mtoto, atumie mtoto ambaye siyo wa kumzaa amlee kama wa kwake na hapo machungu, huzuni na mawazo vitaisha na atamzoa kama wa kwake,” alisema Wastara Juma.
Wengine waliompa pole na kumtakia nguvu kukabiliana na tatizo lake ni pamoja na Jini Kabula, Salome Urassa ‘Thea’, Aisha Bui, Amanda Posh na Baby Madaha ambaye alisema;
“Mtoto siyo mwisho wa maisha, kuna mastaa wengi tu ambao hawana watoto na wanaishi kwa amani kama Oprah, Tyra Banks na wengineo, hivyo siyo ishu kubwa kihivyo, watu waache kumsakama Wema, mimi mwenyewe sina mpango wa kuwa na mtoto.”