Alifunguka kuwa anachopenda ni tabia ya Zari ya kujielewa. Akaendelea kufunguka Zari anajua kutofautisha maisha yao halisi na maisha ya instagram. Kwani baada ya maisha ya instagram ya mapichapicha anajua kuwekeza kwa ajili ya kesho na ni mshauri wake wa mipango ya kimaendeleo.
Pia anasema anazimia ngozi yake Zari Ile mbaya.
Kasema mtarajie mtoto na atakuja kwenye social media kuwaomba mmchagulie Jina siku zikifika maana huyu ni mtoto wa kitaifa.
Amekataa katakata kusema kati ya Zari na Wema nani anayaweza zaidi licha ya kubananishwa sana na watangazaji.
Pia alitumia nafasi hiyo kukanusha uvumi kuwa kagombana na Fela baada ya kumshauri Fela awanunulie gari Yamoto kwani kasema Yamoto wanajengewa kila mtu nyumba yake kitu ambacho ni kikubwa kuliko gari. So huo uvumi ni wa uongo.
Pia alikanusha kuwa na nyama ya kusindika (beef) na Ommy Dimpoz.
Nb: Mimi nimependa hiyo spirit ya Zari muda wa kazi mnapiga kazi, muda wa mapenzi mapenzi na muda wa kuuza sura mnauza sura.
Toa Maoni Yako