Masheikh 50 Waandamana Kwenda Kwa LOWASSA Kumtaka Agombee URAIS 2015.......Wamkabidhi 700,000 Imsaidie Kuchukua Fomu





MASHEKHE wapatao 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania Urais 2015.
  Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu (kulia kwenye picha juu) na Alli Mtumwa (wapili kulia) wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.




Mashekhe hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, wamesema katika salamu zao kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye (Lowassa) hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na wapo nyuma yake katika dua.
  Lowassa amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.
"Ila nataka kuwaahidi, naheshimu sana maneno yenu na nayakubali kwamba siku ikifika kwa taratibu za chama nitachukua fomu," alisema.
Lowassa amesema endapo Mungu atamjalia kushinda uchaguzi, atahakikisha anaendeleza pale Rais Jakaya Kikwete katika nyanja mbalimbali za elimu, afya kilimo kwanza, na huduma nyingine muhimu kwa jamii.
Lowassa amesema "nikifanikiwa nitaanza na elimu, na kufanya elimu kipaumbele chetu kwani elimu ndio msingi wa kila kitu."