Msanii wa Bongo Fleva, Linah akiwa amezungukwa na baadhi ya ndugu na jamaa zake wakati akikata keki iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya sherehe ya kuzaliwa kwake iliyofanyika ndani ya boti.
Msanii wa Hip Hop, Young Killer (kushoto), akiwa amepozi na msanii mwenzake Edo Boy ndani ya Ukumbi wa Paparazi uliopo ndani ya Hoteli ya Slipway.
Mwana FA (wa kwanza kushoto), akiwa katika pozi na Linah, pamoja na Andrew Kusaga.Baadhi ya misosi iliyokuwa imeandaliwa kwenye sherehe hiyo ikiwa mezani.
STAA wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linah’, juzikati alifanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa (bethidei) ndani ya boti iliyokuwa ndani ya maji ya Bahari ya Hindi, jirani na eneo la Hoteli ya Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam.
Wasanii kibao wa muziki wa kizazi kipya walihudhuria sherehe hiyo iliyofana vilivyo.