Mama Mzazi wa aliyekuwa Msanii wa Kizazi Kipya Marehemu Mez B ameelezea Sababu ya Kifo cha Mez B kwamba ni Ugonjwa wa Pneumonia ambao ulikuwa unamumbua siku nyingi.
Akizungumza na DjHaazu Mama yake Mez B amesema Mez b amefariki Mapema leo saa Nne Asubuhi nyumbani kwao huko Dodoma.
Katika Taarifa ya Mama Mzazi wa Mez B amesema kuwa Mez B alilazwa na Kuruhusiwa Mara Kadhaa katika Hospitali ya Mwananchi Dodoma na Juzi juzi Alilazwa kwa takribani Siku 8 na baadae Aliruhusiwa na Madaktari wakampa moyo kuwa Atarudi katika hali yake ya Kawaida.
Vingine alivyovizungumzia Mama Mzazi wa Mez B Ni Pamoja na Kuwa Mez B Hakuwahi Kufanikiwa Kupata Mtoto.