UN kushirikiana na DRC kuwaondoa FDLR


Wanamgambo wa FDLR
Umoja wa Mataifa umesema Rais Joseph Kabila ameahidi kuwa jeshi lake litaungana na la UN katika operesheni dhidi ya waasi wa FDLR.
kikosi cha wanajeshi elfu 20 wa umoja huo watashirikiana na wale wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika kampeni zilizopangwa kuanza karibuni dhidi ya waasi wa Kihutu wa Rwanda.
Wanamgambo wa Kihutu, wanaojulikana kama FDLR, wamekuwa wakilitumia eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kama kambi yao ya kufanya mnashambulizi dhidi ya serikali ya nchi jirani ya Rwanda.
Waasi hao wameshindwa kufikia muda wa mwisho wa kimataifa uliowekwa wiki hii wa kuweka silaha chini na kuondoka katika eneo hilo.