SHEREHE ZA MAULID YA MTUME MUHAMAD (SAW) ZILIVYOFANA JIJINI DAR
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum akitoa mawaidha wakati wa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W) iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbali mbali wa Kiislam wakijumuika pamoja na Waislam wengine kwenye Maulidi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W) iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana ambaye ndie aliekuwa mgeni rasmi akizungumza machache kwenye Maulidi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwaasa watanzania kupendana na kuheshimiana.
Sehemu ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa wamejumuika kwenye Maulidi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W) iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Iran nchini Tanzania,Mh. Mehdi Agha Ja'fari (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana zawadi ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W),wakati Maulidi liyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Iran nchini Tanzania,Mh. Mehdi Agha Ja'fari (kulia) akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum zawadi ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W),wakati Maulidi liyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana wakati wa Maulidi liyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam