Damu na makaratasi vikiwa vimetapakaa kila mahali katika ofisi za jarida la Charlie Hebdo baada ya kuvamiwa na magaidi.
Waandishi na wafanyakazi sita wa jarida la Charlie Hebdo waliouawa Jumatano iliyopita wakiwa katika picha ya pamoja ya mwaka 2000. Waliozungushiwa duara ndiyo waliouawa ambao kutoka kushoto ni Philippe Honore, Georges Wolinski, Bernard Maris na Jean Cabut. Chini yao kwenye ngazi kutoka kushoto nimhariri Stephane Charbonnier na mchora katuni Bernard ‘Tignous’ Verlhac.
Polisi maalum wa Ufaransa (GIPN) wakifanya upekuzi eneo la Corcy, kaskazini mwa Ufaransa kuhusiana na shambulio hilo.
…Wakiwa wamempiga risasi polisi Merabet (42) aliyeinua mkono juu kulia akiomba ahurumiwe. Polisi huyo alikuwa akiwakabili wakati wanatoka kufanya mauaji katika ofisi za jarida hilo.Mmoja wa magaidi (chini kulia) akitokomea baada ya kumuua polisi.
PICHA za mwanzo zimetolewa kuonyesha hali ilivyokuwa katika uvamizi wa ofisi za jarida la vikatuni la Charlie Hebdo jijini Paris, Ufaransa, Jumatano wiki hii ambapo magaidi wawili waliwaua watu 12 na kujeruhi saba.
Magaidi hao wanasemekana walivamia ofisi hizo kutokana na chuki za kutoa vibonzo vyenye kuukashifu Uislam ikiwa ni pamoja na kuchapisha vikatuni vya kumkejeli Mtume Muhammad.
Katika msako mkali unaoendelea nchini Ufaransa, hadi sasa watuhumiwa watatu wamekamatwa kuhusika na shambulio hilo ambao ni Saidi Kouachi (34) na ndugu yake, Cherif Kouachi (32), ambapo Hamyd Mourad (18) kutoka Reims nchini Ufaransa, alijisalimisha mwenyewe baada ya kugundua anatafutwa na poli