Lady Madona apata pigo jingine


MWANAMUZIKI, Lady Madonna amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya nyimbo zake kadhaa kuingia sokoni bila ya ridhaa yake.

Awali mwanamuziki huyo alisema kuwa angeachia nyimbo zake sita kati ya zile zilizopo katika albamu yake ya muziki ikiwa ni kama sikukuu kwa washabiki wa muziki wake.

Lakini imekuja kuwa ni tofauti kwa kuwa mbali na nyimbo hizo sita zimetolewa nyimbo nyingine katika albamu yake ya Rebel Heart.

Nyimbo hizo zimeshaingizwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwa pamoja na wimbo wa Hard Candy aliomshirikisha mwanamuziki Pharrell.

Hii ni mara ya pili kwa msanii huyo kukumbana na hali hiyo ya kuibiwa kazi zake za muziki ambapo mara kwa kwanza ilimtokea na alilifananisha suala hili ni sawa na kuubaka muziki au ni ugaidi kabisa.

Nyimbo zilizochuja ni pamoja na Iconic,Veni Vidi, Vici, Beautiful Scars, Freedom, God Is Love, Hold Tight, Best Night, Inside Out, Tragic Girl, Nothing Lasts Forever, Back That Up (Do It) ft.
Pharrell, Holy Water, Graffiti Heart na Body Shop.