Polisi wakionyesha fedha bandia alizokamatwa nazo bwana Joni Simon.
Mashuhuda waliwaambia OFM kuwa kijana huyo alinaswa katika duka moja la Tigo Pesa lililopo maeneo ya Kona Bar karibu na Hoteli ya kisasa ya Atriums.Baada ya kuwekewa pesa katika simu yake, alitoa ‘mkwanja huo bandia’ na kumkabidhi jamaa wa Tigo Pesa, lakini alizitilia mashaka fedha hizo na kulazimika kumzuia asiondoke kwanza, lakini jamaa huyo akataka kutimua mbio.
Bwana Joni Simon akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Kabla hajafanya hivyo, jamaa wa Tigo Pesa alimrukia na kumshika huku akipiga kelele za kuomba msaada ndipo akaupata kutoka kwa wauza chips walio karibu.Ndipo simu ilipopigwa kwa polisi wa kituo cha Mabatini Kijitonyama ambao wakiongozwa na Kamanda Rashidi wakaingia eneo la tukio mara moja lakini walilazimika kutumia bunduki kumtisha ili kumtuliza kijana huyo na kumtia mbaroni.Baada ya kumpekua walimkuta na kiasi cha zaidi ya shilingi laki mbili, zote zikiwa bandia na waliondoka naye kuelekea kituoni kwa mahojiano zaidi kabla ya hatua nyingine za kisheria kufuata.
RPC Wambura.
Tukio hilo limetokea siku chache tu baada ya mtu mmoja huko mkoani Mwanza, kukamatwa akiwa na kiasi cha shilingi milioni 400 za Kitanzania, ambazo pia ni bandia, zilizokusudiwa kuingizwa katika mzunguko wa fedha