Huyu ndie inasadikiwa alifanya tukio hilo la kijasusi anaejulikana kwa jina la Haron Monis rekodi zake za uhalifu zinajulikana sana na polisi wa Australia
Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott amesema mtu mwenye bunduki aliyehusika na utekaji nyara watu katika mkahawa mmoja jijini Sydney alikuwa akijulikana kwa vyombo vya serikali na alikuwa na historia ndefu ya uhalifu, akiwa amegubikwa na itikadi kali za kidini na kuwa na hitilafu ya akili.
Watu wawili waliuawa, pamoja na Jasusi aliyejihami kwa bunduki baada ya makomandoo kuvamia mkahawa huo uliopo eneo la kibishara jijini Sydeney, na kumaliza tukio la utekaji nyara lililodumu kwa saa kumi na sita.Watu wanne walijeruhiwa katika tukio hilo, ikiwa ni pamoja na askari polisi aliyepigwa na vipande vya risasi.
Raia wawili waliofariki kwenye tukio hilo la kigaidi wametajwa kuwa ni mwanamke mwanasheria mwenye watoto watatu anaejulikana kwa jina la Katrina Dawson, 38 na meneja wa mgahawa huo wa Lindt bwana Tori Johnson, mwenye umri wa miaka 34
Mtu huyo mwenye silaha alitambuliwa kuwa mkimbizi kutoka Iran, aliwashiklia mateka watu kadha katika mkahawa wa Lindt.
Video hii inaonesha wakati Polisi wa Australia walipovamia jengo la lindt caffe n
Eneo la katikati ya jiji la Sydney lilifungwa wakati mtu mwenye silaha alipowashikilia mateka watu mapema Jumatatu, akiwalazimisha baadhi yao kunyanyua juu dirishani bango jeusi la Kiislam katika mkahawa wa Lindt.
Waziri Mkuu Tony Abbott amesema "tukio la kutisha" katika mkahawa kulikuwa na "hali ya kutisha kuzidi maelezo" na kulikuwa na "kitu cha kujifunza" kutoka tukio hili la kigaidi".
"matukio haya yanaonyesha kuwa hata kwa nchi yenye uhuru, yenye uwazi na ukarimu kama nchi yetu, bado inakabiliwa na vitendo vya ghasia zenye msukumo wa kisiasa lakini pia yanaonyesha kuwa tuko tayari kukabiliana nayo," aliwaambia waandishi wa habari.
Baadhi ya watu waliojeruhiwa katika uvamizi uliofanywa na raia wa Iran na kuwateka nyara watu ndani ya mgahawa