MWANASHERIA MKUU WA SEREKALI, JAJI WEREMA AJIUZULU


Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema (pichani) amejiuzulu nafasi yake na tayari amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Kikwete.
Rais Kikwete asema amepokea barua yake na kumshukuru kwa ushirikiano aliouonyesha katika kipindi cha utumishi wake.

Sababu ya kujiuzulu ni kwamba ushauri alioutoa kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka vizuri.